Dawa ya meno kwa mfungaji


Swali: Je, dawa ya meno inamfunguza mfungaji au hapana?

Jibu: Dawa ya meno haifunguzi mfungaji. Hali kadhalika Siwaak, kusafisha kwa sabuni au kitu kingine. Vyote hivi havimfunguzi mfungaji. Lakini mtu atahadhari kusiteremke kitu kwenye koo yake. Ni mamoja ni dawa ya meno au kitu kingine. Ahakikishe kusiingie kitu ndani ya koo yake. Ama kusafisha meno kwa dawa ya meno, sabuni au aina nyenginezo halafu baada ya hapo mtu akatema, hakumdhuru mfungaji. Ikiwa atakusudia kumeza kitu katika hivyo, swawm yake inaharibika. Upande mwingine kukiteremka kitu kwenye koo yake pasi na kukusudia, kikamshinda au akasahau hakiharibu swawm yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.binbaz.org.sa/noor/9787
  • Imechapishwa: 04/06/2017