Dawa ya kuzuia uzazi bila mume kujua

Swali: Baadhi ya wanawake hutumia madawa ya kuzuia mimba katika ule mwaka wa kwanza wa ndoa bila ya waume zao kujua. Wanafanya hivo ili wasishike mimba na pia kwa kuogopa kutoelewana na waume zao. Je, inajuzu kwao kufanya hivo?

Jibu: Haijuzu kufanya hivo isipokuwa kwa ridhaa ya mume wake. Ni haki yake. Haijuzu kwake kutumia dawa ya kuzuia mimba pasi na idhini yake. Vilevile haijuzu kutumia kitu kitachofunga kizazi kabisa, isipokuwa kitu cha kuzuia kwa muda fulani wakati wa haja kukiwemo ugonjwa au kutoweza. Katika hali hii anaweza kutumia dawa inayozuia kwa muda. Ama dawa inayofunga kizazi kabisa haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (7) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–15041434.mp3
  • Imechapishwa: 17/12/2016