Dawa ya kinywaji ya alcohol dhidi ya ugonjwa wa macho


Swali: Mama yangu ni mgonjwa kwenye jicho lake. Daktari mmoja anamshauri kunywa mimea iliyochanganyikana na alcohol. Asipofanya hivo basi atalazimika kufanyiwa upasuaji. Je, inajuzu kwake kunywa?

Jibu: Alcohol ni uchawi. Haijuzu kujitibu kwa uchawi. Kuna madawa mengine:

“Allaah hakuteresha ugonjwa wowote isipokuwa ameteremsha vilevile dawa yake; amejua yule mwenye kujua na hakujua yule ambaye hakujua.”[1]

Apeleke suala lake kwa wenye uzoefu na watambuzi na amuombe Allaah du´aa (Subhaanahu wa Ta´ala) amponye.

[1] at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Awsatw” (3/75). Swahiyh kwa mujibu wa Ibn ´Abdil-Barr i ”at-Tamhiyd” (5/283).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (61) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid-%2029%20-0%206-1438.mp3
  • Imechapishwa: 06/08/2017