Swali: Ni ipi hukumu ya kuchukua mihadhara kwa video camera kwa hoja ya kwamba itatumwa katika nchi za mbali kama mfano wa Marekani?

Jibu: Baraka zinatoka kwa Allaah. Kunaweza kusemwa maneno machache katika kikao kidogo na yakafika ulimwenguni kote. Vilevile watu au Hizbiyyuun wanaweza kuyakariri maneno na yakapotelea hewani na yasiwe na athari yoyote. Naonelea kuwa picha ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila mtengeneza picha yuko Motoni. Ataambiwa aipulizie roho kila picha aliyotengeneza na kuadhibiwa kwayo Motoni.”

at-Tirmidhiy amepokea katika “al-Jaamiy´” kupitia kwa Abu Hurayrah ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Siku ya Qiyaamah kuna shingo itatoka Motoni. Itakuwa na macho mawili yanayoona, masikio mawili yanayosikia na ulimi unaozungumza na kusema: “Mimi nimepewa kazi ya kusimamia watu aina tatu; kila ambaye ni mwenye kiburi mkaidi, ambaye alimfanyia Allaah mungu mwengine na ambaye ni mtengeneza picha.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Malaika hawaingii katika nyumba ilio na picha wala mbwa.”

Mizunguko ya kielimu imebarikiwa kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hawakusanyiki watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah ambapo wanasoma Kitabu cha Allaah na wanadarasishana baina yao isipokuwa Allaah huwateremshia utulivu, Malaika wanawazunguka na rehema zinawateremkia.”

Hata hivyo hao watengeneza picha wanawafukuza Malaika mbali kutokamana na vikao.

Kitendo hichi ni dhambi. Ni lazima kikemewa kwa kiasi cha uwezo. Usizue fitina. Ikiwa huwezi kukataza dhambi hiyo basi toka hapo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu, basi ayazuie kwa mkono wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa mdomo wake. Asipoweza, basi afanye hivo moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=h9BUSNO053U
  • Imechapishwa: 15/04/2018