Swali: Je, inajuzu kufanya darsa asubuhi ya siku ya ijumaa? Nimesikia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mizunguko ya kielimu siku ya ijumaa.

Jibu: Si jambo zuri. Darsa zinatakiwa kuwa ima baada ya swalah ya ijumaa au siku nyingine isiyokuwa ya ijumaa. Ama kabla ya swalah, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mizunguko ya kielimu siku ya ijumaa kwa sababu inasumbua kutokamana na ijumaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017