Swali: Mimi ni imamu wa msikiti na huwazungumzisha maamuma baada ya swalah ya ´Aswr na ´Ishaa kwa kuendelea na pasi na kubagua siku miongoni mwa siku za wiki. Lakini wapo baadhi ya watuwazima ambao wananikemea kuongea siku ya ijumaa kwa hoja kwamba wanachuini wao waliokutana nao wanalichukia hilo. Je, kuna hukumu yoyote ya Kishari´ah?

Jibu: Ikiwa darsa anazotoa ni kwa njia ya mawaidha, basi hatakiwi kuwatolea watu kila siku akawachokesha. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akizichunga hali za Maswahabah zake katika mawaidha.

Ama ikiwa ni darsa za kielimu, hakuna neno akaendelea kufanya kila siku. Wanachuoni wetu ambao walikuwa siku ya ijumaa hawawafundishi watu, walikuwa wakifanya hivo kwa hoja wasiwachoshe watu. Kwa sababu watu tayari wamekwishasikia Khutbah ya ijumaa na wametosheka nayo kiwaidhika na kuelewa. Kwa ajili hiyo wanachuoni wetu ambao tulikutana nao walikuwa hawawaongeleshi watu siku ya ijumaa baada ya ´Aswr kwa kutosheka na Khutbah ya ijumaa.

Lakini mtu akifanya hivo hakuna neno. Kwa msemo mwingine mtu akawa anawasomesha watu kila alasiri, kukiwemo siku ya ijumaa, hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1228
  • Imechapishwa: 12/04/2019