Damu ya mwanadamu ni safi isipokuwa yenye kutoka kupitia njia mbili

Swali: Ni ipi hukumu iwapo damu yenye kutoka kwenye kidonda cha mkononi itaingia kwenye nguo yangu? Je, damu ni najisi au hapana? Ni damu ipi ambayo inanajisi?

Jibu: Mtu akiswali ndani ya nguo ambayo imepatwa na damu kutoka mkononi mwake, basi swalah yake ni sahihi. Kwa sababu inayomtoka mtu sio najisi isipokuwa ile inayotoka kupitia katika tupu ya mbele au ya nyuma. Damu inayotoka mapuani ni safi. Damu inayotoka kwenye kidonda kwa sababu mtu amekanyaga kigaya, msumari na vinginevyo ni safi. Hakuna, si katika Qur-aan wala Sunnah, ya kwamba damu ya mwanadamu ni najisi. Isipokuwa tu ile inayotoka kupitia katika tupu ya mbele au ya nyuma. Hii ndio najisi. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha mwanamke mwenye hedhi aoshe damu yake. Ama damu nyingine hapakuja maamrisho ya kuiosha. Maswahabah vitani walikuwa wakiswali wakiwa na madonda yao. Damu ya kwenye vidonda ni nyingi vitani. Kuhusu kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuosha uso wake kuondosha damu wakati alipoumizwa katika Uhud, sio dalili ya unajisi. Huku ni kuondosha tu damu kwa sababu amechafuka na hataki watu wamuone yuko na damu.

Kwa kufupiza ni kwamba damu ya mwanadamu ni safi isipokuwa ile inayotoka kupitia katika tupu ya mbele au ya nyuma. Hilo ni kutokana na kuenea kwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Muumini hanajisiki.”

Katika Hadiyth nyingine imekuja:

“Chenye kuonekana kutoka kwa hai ni kama mfu.”

Maiti ya mwanadamu ni safi au najisi? Ni safi. Lakini haitakikani kwa mtu akaacha athari ya damu katika mwili wake. Bali anachotakiwa aioshe kwa sababu wakiudhike kwa kumtazama.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1221
  • Imechapishwa: 03/09/2019