Damu kutoka puani katikati ya swalah


Swali: Baba yangu hutokwa na damu puani mwake na anakuwa na leso mkononi mwake kwa ajili ya kuzuia. Afanye nini katikati ya swalah? Je, kuna kitu juu yake endapo ataswali na huku damu yamtoka?

Jibu: Nimechopata kufahamu katika swali ni kwamba ni jambo lenye kuendelea. Hakuna neno juu yake. Hakuna juu yake neno juu ya damu hii yenye kumtoka. Kama alivyosema achukue leso na apanguse pua yake. Lakini ikimtokea katikati ya swalah yake atoke ndani ya swalah au aendelee? Tunasema ikiwa hilo linamshughulisha basi atoke kwa kuwa ni mwenye udhuru. Ikiwa halimshughulishi aendelee.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1614
  • Imechapishwa: 25/09/2018