Swali: Mwanamke kabla ya kujifungua anakuwa na alama na anatokwa na maji maji. Na wakati mwingine hali inaendelea namna hii siku mbili mpaka zaidi. Ipi hukumu ya Swalah wakati wa hali hiyo?

Jibu: Ikiwa ni kabla ya kujifungua, haidhuru In Shaa Allaah. Anatakiwa kuswali. Na ikiwa ni damu, huzingatiwa kuwa ni damu katika damu ya uzazi (nifasi). Hapo Swalah itasimama kwake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2594
  • Imechapishwa: 07/03/2018