Damu inayomtoka mswaliji puani

Swali: Damu inayotoka puani wakati wa swalah inavunja swalah?

Jibu: Damu inayotoka puani ikiwa ni ndogo basi haki isiyokuwa na shaka ndani yake ni kwamba haichengui wudhuu´ na wala haibatilishi swalah. Ile damu ndogo inayoingia nguoni ni yenye kusamehewa.

Ikiwa ni damu nyingi wanachuoni wametofautiana juu yake. Wako waliosema kuwa azibe pua yake na wala haibatilishi swalah. Miongoni mwao wako waliosema kuwa inabatilisha swalah ikiwa ni nyingi. Hivyo basi atalazimika kuondoka ndani ya swalah na kuosha pua yake na ajitahidi kuimaliza damu hii kisha aanze swalah yake upya. Maoni haya ndio salama na bora zaidi. Kwa sababu kufanya hivo kuna kuichunga swalah zaidi, ni kutoka nje ya tofauti na jengine ni kwa sababu damu ni najisi. Ile damu ndogo inasamehewa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4141/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%AF%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B0%D9%8A-%D9%8A%D9%86%D8%B2%D9%81-%D8%A7%D8%AB%D9%86%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9
  • Imechapishwa: 09/08/2020