Damu inayokatika katika siku za hedhi

Swali: Ni ipi hukumu damu inapokatika katikati ya siku za hedhi kisha inaendelea kama siku moja au mbili. Je, aswali katika siku hii moja au mbili au ni katika hedhi?

Jibu: Huyu inawezekana alifanya haraka kabla ya kukatika damu. Maadamu ni kama damu ya hedhi na iko karibu nayo [katika sifa zake], hakuna baina yake na hiyo damu isipokuwa kuna mapumziko madogo tu, basi ni katika hedhi. Alifanya haraka. Anachukuliwa kuwa ni mwenye kukamilisha siku zake za hedhi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14857
  • Imechapishwa: 23/09/2020