Damu inaendelea kutoka zaidi ya siku ishirini

Swali: Mimi ni mwanamke mtumzima. Mwanzoni nilikuwa nikipata hedhi kwa muda wa siku saba. Miaka kumi iliyopita nikapatwa na maradhi na damu ya hedhi ikawa inatoka takriban kwa siku ishirini na tano, ishirini na wakati mwingine siku kumi na tano. Nikae siku ngapi pasi na kuswali? Wakati mwingine kabla ya kutokwa na damu naona kama msitari mwekundu. Je, niswali wakati ninapoona msitari huu au hapana?

Jibu: Midhali damu inaendelea kwa siku ishirini na tano au ishirini, basi hii ni damu ya ugonjwa. Hivyo anatakiwa kurudi katika ada yake ya mwanzo kabla ya kupatwa na maradhi haya. Baada ya hapo ajisafishe na kuswali. Hivo ndivo alivyoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwanamke mwenye damu ya istihadhah ambaye kabla ya hapo alikuwa na ada aliyozowea, basi arudi katika ile ada yake kisha aoge na kuswali japokuwa damu itakuwa bado ni yenye kutoka. Damu hiyo haimdhuru. Kadhalika mwanamke atapoona uchafuchafu au rangi ya manjano kabla ya kuanza kwa hedhi hayazingatiwi. Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Tulikuwa hatuzingatii uchafuchafu na manjano baada ya kusafika chochote.”

Katika tamko la al-Bukhaariy imekuja:

“Tulikuwa hatuzingatii uchafuchafu na manjano baada ya kusafika chochote.”

Pasi na kufungamanisha na baada ya kusafika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (50) http://binothaimeen.net/content/1148
  • Imechapishwa: 22/06/2019