Damu inaendelea kutoka baada ya siku 40 kwa mtazamo wa Ibn ´Uthaymiyn

Swali: Mwanamke amemaliza siku arubaini za muda wa kipindi cha damu yake ya uzazi kisha baada ya siku arubaini akatokwa na damu. Ni ipi hukumu? Naomba kuwekewa wazi na faida?

Jibu: Maoni yenye nguvu ni kwamba midhali damu bado ni yenye kuendelea kutoka, basi ni wajibu kwake kubaki katika damu yake hiyo ya uzazi mpaka akamilishe siku sitini. Akikamilisha siku sitini na damu ikaendelea kutoka, chenye kuzidi juu ya siku sitini kikikutana na ada yake basi hiyo ni hedhi, na kisipokutana na ada yake ya hedhi, basi hiyo ni damu fasidi. Katika hali hiyo atatakiwa kuoga na kuswali na atakuwa ni halali kwa mume wake.

Akisafika kabla ya siku arubaini, basi ni wajibu kwake kuoga na kuswali. Inafaa vilevile kwa mume wake kumwingilia japokuwa ni kabla ya siku arubaini midhali ametwaharika. Kwa sababu ikiwa swalah imehalalika kwake, ambayo ni kubwa zaidi kuliko mume wake kustarehe naye, basi mume wake kustarehe naye ni jambo lina haki zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (56) http://binothaimeen.net/content/1274
  • Imechapishwa: 07/10/2019