Dalili za maimamu na Ahl-us-Sunnah kuthibitisha kuwa Allaah yuko juu:

Mosi: Dalili ya kiakili kwa njia ya utafiti na mgawanyiko. Njia hii kwa watu wa mantiki na Ahl-us-Usuwl ni yule mtoaji dalili kuweka kikomo ya vile vigawanyo ambavyo vinaingia akilini kisha baada ya hapo akakiangusha kimoja baada ya kingine na kubakiza yale yaliyosimama juu ya dalili. Dalili yenyewe ni kwa kusema ifuatavyo: Allaah alipoumba viumbe ni lazima ipatikane moja kati ya yafuatayo:

a) Aliviumba ndani ya dhati.

b) Aliviumba nje ya dhati Yake.

c) Aliviumba si ndani ya dhati Yake wala nje Yake.

Hivi ndivyo vigawanyo vinavyoingia akilini.

Kuhusiana na kigawanyo cha kwanza kusema kuwa aliviumba ndani ya dhati Yake ni batili kwa maafikiano baina yetu na wapinzani wetu. Kwa sababu hilo litalazimisha kwa Mola [kwa dhati Yake] awe ni sehemu vilevile ya matukio, mabadiliko na takataka. Hii ni kauli ya Huluuliyyah na ni kufuru.

Hakuviumba si ndani ya dhati Yake wala nje Yake. Hili haliingii akilini. Kwa sababu hili linalazimisha kumkanusha Yeye (Ta´ala) na kutokuwepo kikamilifu. Huku ni kumsifu kwa sifa za mambo mawili yenye kujigonga na kutokuwepo. Hii ni kauli ya Mu´attwilah, Jahmiyyah na wakanushaji. Hii ni kufuru pia.

Kigawanyo kinachosema kuwa aliviumba nje ya dhati Yake. Hili limelazimisha kutengana. Katika hali hiyo italazimisha awe juu ya viumbe Vyake na amelingana juu ya ´Arshi Yake. Kwa sababu ni lazima ipatikane moja katika haya:

– Awe ametangana nao kwa kuwa juu yao.

– Awe chini yao.

– Mbele yao.

– Nyuma yao.

– Upande wao wa kulia.

– Upande wao wa kushoto.

Linaloendana na akili ni Yeye Allaah kuwa juu kwa sababu miongoni mwa Sifa Zake anazosifika nazo ni ukamilifu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/411-412)
  • Imechapishwa: 19/05/2020