Dalili za kiakili za Ahmad ya kwamba Allaah ametengana na viumbe Wake

Ukitaka kujua kuwa Jahmiy anamsemea uongo Allaah ni pale aliposema kuwa Allaah yuko kila mahali, hawi sehemu pasi na kwengine, muulize:

”Si kulikuwepo wakati ambapo Allaah alikuwepo na hakukuwepo kitu kingine?”

Atasema:

”Ndio.”

Mwambie:

”Alipowaumba viumbe, aliwaumba ndani Yake au nje Yake?”

Hapa hawezi kujibu isipokuwa majibu matatu:

1 – Akisema kuwa aliwaumba viumbe ndani Yake, anakufuru kwa kuwa hii ina maana kwamba majini, watu na mashaytwaan wako ndani ya Allaah.

2 – Akisema aliwaumba nje Yake kisha akaingia ndani yao, anakufuru kwa kuwa itakuwa na maana kwamba Allaah ameingia ndani ya kila sehemu zote zilizo na uchafu na taka.

3 – Akisema aliwaumba nje Yake pasi na kuingia ndani yao, anarudi katika maoni yake – na haya ndio maoni ya Ahl-us-Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 155-156
  • Imechapishwa: 13/04/2017