Dalili ya mjamzito na mnyonyeshaji kulipa madeni yao na kulisha

Swali: Baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa mwanamke mjamzito na mnyonyeshaji wakikhofia juu ya mtoto haiwalazimikii juu yao kitu isipokuwa kulipa tu na hakuna dalili ya kulisha. Unasemaje juu ya hili?

Jibu: Mjamzito na mnyonyeshaji hawakutajwa katika Qur-aan [kuhusu rukhusa ya kula na kulipa siku nyingine]. Kumetajwa mgonjwa na msafiri tu na mzee pia asiyeweza kufunga. Hii ni Fatwa ya Maswahabah, kama Ibn ´Umar na wengineo. Hili limepokelewa kutoka kwa Maswahabah. Halikukanushwa. Sio lazima kuwepo dalili katika Qur-aan na Sunnah, bali matendo na Fataawaa za Maswahabah zinatendewa kazi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-02-09.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014