Dalili Ya Kujuzu Kwa Filamu/Tamthiliya


Swali: Wanaojuzisha filamu na maigizo ya michezo kwa kitendo cha Malaika kujigeuza umbila la mwanaadamu wana mtazamo wa sawa kwa hilo?

Jibu: Huku ni kuyapotosha maneno mahala pake. Malaika wanajigeuza kwa umbile la mwanaadamu kwa kuwa sisi hatuwezi kuwaona. Kuhusu filamu – je, wewe huwezi kumuona yule muigizaji mpaka ajigeuze sura ya [sauti haiko wazi] au ngedere? Wewe huwezi kumuona mwanaadamu? Huku ni kuyapotosha maneno mahala pake. Hii sio dalili ya kujuzu kwa filamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (16) http://alfawzan.af.org.sa/node/2059
  • Imechapishwa: 30/04/2017