Swali: Anauliza juu ya dalili ya yule ambaye amezembea kulipa deni la Ramadhaan mpaka akaingiliwa na Ramadhaan nyingine kwamba ni wajibu pamoja na kulipa atoe kafara vilevile?

Jibu: Aliyechelewesha Ramadhaan mpaka kukaingia Ramadhaan nyingine ikiwa amefanya hivo kwa udhuru, kama ile ugonjwa, na hakupona kwa kiwango cha yale masiku anayodaiwa au alikuwa msafiri na hakujaaliwa kupata muda wa kulipa yale masiku anayodaiwa, anatakiwa kulipa masiku anayodaiwa na hakuna kingine kinachomlazimu. Lakini akizembea kwa yeye kupona kwa kiwango cha yale masiku anayodaiwa na akawa hakufunga mpaka akaingiliwa na Ramadhaan ya pili, huyu anatakiwa kufunga siku za Ramadhaan anazodaiwa pamoja na kutoa kafara kwa kulisha kwa kila siku moja masikini. Hivi ndivyo  walivyofutu baadhi ya Maswahabah. Hata hivyo kuna wanachuoni wenye kuonelea kuwa hakuna kinachomlazimu isipokuwa tu kulipa masiku yake. Lakini baadhi ya Maswahabah wamefutu ya kwamba anatakiwa kulipa pamoja vilevile na kulisha kwa kila siku moja masikini. Kwa sababu ya kule kuzembea kwake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa//index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=67889&audiotype=lectures&browseby=speaker
  • Imechapishwa: 07/08/2017