Dalili ya Jamaa´t-ut-Tabliygh ya kufanya Da´wah bila elimu

Swali: Nini maana ya maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّـهُ

“Mcheni Allaah na Allaah anakufunzeni.”[1]?

Je, inasihi hii kuwa ni dalili inayowasapoti baadhi ya makundi, kama vile Jamaa´at-ut-Tabliygh, ambao wanatoka kulingania pasi na elimu kwa kutumia hoja Aayah hii?

Jibu: Aayah hii iko dhidi yao. Inasema:

وَاتَّقُوا اللَّـهَ

“Mcheni Allaah.”

Miongoni mwa kumcha Allaah ni mtu kujifunza elimu na asizungumze pasi na elimu, asimsemee Allaah pasi na elimu na asilinganie katika Bid´ah na mambo mepya. Huyu hakumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

[1] 02:282

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/node/13189 Tarehe: 1432-01-18/2010-12-24
  • Imechapishwa: 26/05/2022