Dalili ya alama ya jiwe kwenye kaburi

3060- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kwalo nitaweza kulijua kaburi la ndugu yangu na kuwazika ndugu zangu wanaokufa karibu naye.”

Ameipokea Abu Daawuud (3206), kupitia kwake al-Bayhaqiy (3/412) na Ibn Shubbah katika ”Taarikh-ul-Madiynah” (1/102) kupitia kwa Kathiyr bin Zayd al-Madaniy, kutoka kwa al-Muttwalib ambaye ameema:

“Wakati ´Uthmaan bin Madh´uun alipofariki na jeneza lake likatolewa nje na kuzikwa, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha mtu mmoja amletee jiwe. Mwanamume yule hakuweza kulibeba jiwe lile ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasimama na akakunja mikono yake.” Kathiyr amesema: “al-Muttwalib amesema: Yule aliyenieleza hayo kuhusu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Niliona weupe wa mikono ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipokunja mikono yake. Halafu akalinyanyua, akaliweka karibu na kichwa chake na akasema:

“Kwalo nitaweza kulijua kaburi la ndugu yangu na kuwazika ndugu zangu wanaokufa karibu naye.”

Cheni ya wapokezi ni nzuri na iliokamatana.

Shaafi´iyyah wanatumia Hadiyth hii kama dalili juu ya kuweka alama ya jiwe au kitu kingine karibu na kichwa cha maiti. Hoja yao ni kwamba kaburi linatakiwa kutambulika na kutembelewa. Mi pia naona kwamba likiwekwa alama likatambulika halitofanyiwa kikao na wala halitokanyagwa na viatu. Abu Daawuud ameiwekea kichwa cha khabari kwa kusema:

“Mlango unaozungumzia kuwakusanya maiti ndani ya kaburi moja na kaburi litambuliwe.”

al-Bayhaqiy amesema:

“Mlango unaozungumzia kulifanya kaburi likatambulika au kuliweka alama ya jiwe au kitu kingine.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (7/1/166)
  • Imechapishwa: 23/05/2019