al-Khaliyliy amesema:

“Kuhusu dalili za kinakili – za wanaopinga kuonekana kwa Allaah – baadhi zinapatikana katika Qur-aan na zingine katika Sunnah.”[1]

Kisha akasema:

“Katika Qur-aan ni maneno Yake (Ta´ala):

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ

“Macho hayamzunguki na Yeye ndiye anayazunguka macho yote – Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari wa yote.”[2]

Halafu akasema:

“Dalili hapa ni kwamba (Ta´ala) amejisifu kuwa macho hayamdiriki. Kudiriki maana yake ni kuona. Ikapata kubainika kuwa kutoonekana kwa macho ni sifa ya kidhati yenye kulazimiana Naye (Ta´ala). Lau kungelikuwa kipindi anaonekana basi kujisifu Kwake kungeondoka na mambo yakishakuwa hivo inageuka kuwa kinyume chake ambacho ni kulaumika – Allaah ametakasika na hilo.”

Akaendelea kusema:

“Kwa upande mwingine ni kwamba [hapa] Allaah anaelezea sifa miongoni mwa sifa Zake na maelezo ya Allaah hayabadiliki. Lau ingelibadilika basi kubadilika kwake ingelikuwa ni kumkadhibisha:

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا

“Na nani aliye mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah?”[3]

Hivi ndivyo vyanzo vya al-Khaliyliy kupinga kuonekana Allaah Aakhirah kwa kutumia dalili za Qur-aan, kama anavyodai. Wewe mwenyewe unaona kuwa katika Aayah tukufu hakuna dalili inayokanusha kuonekana kwa Allaah. Bali Aayah ina haki zaidi ya kuthibitisha kuonekana. Kudiriki sio kuonekana[4]. Kunaweza kupatikana kuonekana na kusipatikane uzungukaji.

al-Khaliyliy alirejea kwenye tafsiri ya Ibn Jariyr juu ya Aayah lakini hata hivyo hakuchukua maoni ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye ndiye mwenye kutarjumu Qur-aan wala ya Qataadah. Alichofanya ni kuchukua Aayah zinazokanusha Allaah kuonekana duniani na akazifanya kuwa ndio zinakanusha kuonekana Allaah duniani na Aakhirah, kama tulivyotangulia kutaja baadhi ya hayo.

[1] Uk. 68

[2] 06:103

[3] 04:122

[4] Tazama http://www.wanachuoni.com/content/radd-juu-ya-utata-wa-wenye-kupinga-kuonekana-kwa-allaah-aakhirah-5

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 98-99
  • Imechapishwa: 14/01/2017