Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke mwenye hedhi kugusa msahafu na kusoma ndani yake?

Jibu: Sijui kama kuna makatazo yoyote ya kufanya hivi. Ama Kauli Yake (Ta´ala):

لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ

“Hawaigusi isipokuwa waliotwahara.” (56:79)

Makusudio ni Malaika, kama Alivyosema (Subhaanahu wa Ta´ala) katika Aayah ya ash-Shu´araa:

  وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ الشَّيَاطِينُ وَمَا يَنبَغِي لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ

“Na wala hawakuteremka nayo [Qur-aan hii] mashaytwaan na wala haipasi kwao na wala hawawezi.” (26:210)

Na amesema Imaam Maalik katika “al-Mu´attwah”:

“Kauli Yake (Ta´ala): Inafasiriwa na Aayah ya ´Abasaa:

كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ بِأَيْدِي سَفَرَةٍ كِرَامٍ بَرَرَةٍ

“Sivyo katu! Hakika hizi ni Ukumbusho. Basi atakaye akumbuke. [Zimeandikwa] katika swahifa zilizokirimiwa. Zimetukuzwa na zimetwaharishwa. [Zinazobebwa] mikononi mwa waandishi, watukufu na watiifu.” (80:11-16)

Yaani hawakuteremka nayo mashaytwaan, isipokuwa imeteremka na Malaika.

“Mikononi mwa waandishi, watukufu na watiifu.”

nao ni Malaika.

Na amepokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake:

“Ibn ´Abbaas alikuwa haonelei mwenye janaba tu kusoma Qur-aan.”

Hakuna ubaya kwa hili – In Shaa Allaah. Tumebakia na Hadiyth nyingine inayosema:

“Haigusi Qur-aan isipokuwa aliye msafi.”

Hadiyth hii katika njia zake zote, kuna mtu dhaifu ndani yake naye ni Swaalih bin Hujjiyah. Lakini hata hivyo, tunachukua kama alivyoifasiri Imaam ash-Shawkaaniy katika “Nayl-ul-Awtwaar”: Maana yake ni:

“Haigusi Qur-aan isipokuwa muislamu.”

Abu Hurayrah kapokea pia kuwa:

“Hakika ya muislamu hajanasiki.”

Hivyo, maana yake ni kuwa haigusi [Qur-aan] isipokuwa muislamu tu. Kwa dalili ya kwamba, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataza kusafiri na Qur-aan katika ardhi miji ya makafiri.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.net/default_ar.aspx?id=8107
  • Imechapishwa: 05/03/2018