Dalili kuwa mwanamke mwenye hedhi anaruhusiwa kugusa msahafu na kusoma


Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke mwenye hedhi kugusa msahafu na kusoma ndani yake?

Jibu: Sijui kama kuna makatazo yoyote ya kufanya hivi. Ama Kauli Yake (Ta´ala):

لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ

“Hawaigusi isipokuwa waliotwahara.” (56:79)

Makusudio ni Malaika, kama Alivyosema (Subhaanahu wa Ta´ala) katika Aayah ya ash-Shu´araa:

وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ الشَّيَاطِينُ وَمَا يَنبَغِي لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ

“Na (wala) hawakuteremka nayo (hii Qur-aan) mashaytwaan. Na (wala) haipasi kwao (kuteremka na Qur-aan) na wala hawawezi.” (26:210)

Na amesema Imaam Maalik katika “al-Mu´attwah”:

“Kauli Yake (Ta´ala): Inafasiriwa na Aayah ya ´Abasaa:

كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ بِأَيْدِي سَفَرَةٍ كِرَامٍ بَرَرَةٍ

“Sivyo katu! Hakika (hizi Aayah za Qur-aan) ni ukumbusho. Basi atakaye akumbuke. (Zimeandikwa) Katika swahifa zilizokirimiwa (Al-Lawh Al-Mahfuwdh). Zimetukuzwa na zimetwaharishwa. (Zinazobebwa) Katika mikono ya (Malaika) waandishi. Watukufu (na) watiifu.” (80:11-16)

Yaani hawakuteremka nayo Mashaytwaan, isipokuwa imeteremka na Malaika. “Katika mikono ya waandishi”, nao ni Malaika. “Watukufu (na) watiifu.” Na amepokea al-Bukhaariy katika Swahiyh yake:

“Ibn ´Abbaas alikuwa haonelei mwenye janaba tu kusoma Qur-aan.”

Hakuna ubaya kwa hili In Shaa Allaah. Tumebakia na Hadiyth nyingine inayosema:

“Haigusi Qur-aan isipokuwa aliye Twahara.”

Hadiyth hii katika njia zake zote, kuna mtu dhaifu ndani yake naye ni Swaalih bin Hujjiyah. Lakini hata hivyo, tunachukua kama alivyoifasiri Imaam ash-Shawkaaniy katika “an-Nayl al-Awtwaar”: Maana yake ni:

“Haigusi Qur-aan isipokuwa Muislamu.”

Abu Hurayrah kapokea pia kuwa:

“Hakika ya Muislamu hajanasiki.”

Hivyo, maana yake ni kuwa haigusi (Qur-aan) isipokuwa Muislamu tu. Kwa dalili ya kwamba, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataza kusafiri na Qur-aan katika ardhi (miji) ya makafiri.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.net/default_ar.aspx?id=8107
  • Imechapishwa: 05/03/2018