Swali: Vipi ataraddiwa yule mwenye kusema kwamba Hijaab ni ile inayofunika nywele peke yake khaswa kwa kuzingatia kwamba chaneli nyingi za satelaiti zinawaleta wanawake wenye kutoa fatwa ambao wanasema kuwa kufunika uso sio jambo la wajibu?

Jibu: Watu hawa hawana elimu. Dalili ziko wazi kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Kuna vitabu vimeandikwa kuhusu maudhui haya. Miongoni mwa vitabu hivyo ni kitabu cha muheshimiwa Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn. Ni kitabu kizuri kinachozungumzia Hijaab[1]. Mtu arejee huko kuhusiana na dalili. Ameweka wazi masuala haya kwa Aayah ya “al-Ahzaab” na maneno ya wanachuoni wa tafsiri ya Qur-aan wakifasiri Aayah hii ya “al-Ahzaab”:

وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ

“Mnapowauliza haja, basi waulizeni nyuma ya pazia.”[2]

Hadiyth kunako jambo hili ziko wazi.

Ama kuhusu watu hawa ambao wanatoa fatwa katika chaneli za satelaiti hawana elimu. Baadhi yao ni wenye maradhi ya nyoyo na wanafuata matamanio yao.

[1] Hiki hapa https://firqatunnajia.com/wp-content/uploads/2016/10/al-Hijaab-Imaam-Ibn-%C2%B4Uthaymiyn-.pdf

[2] 33:53

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (09) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191370#219699
  • Imechapishwa: 09/03/2019