Swali: Ni ipi dalili ya kutojuzu kujumuisha baina ya swalah ya ´Aswr na Ijumaa?

Jibu: Kwa kuwa halikufanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala na yeyote katika Maswahabah zake. Kulinyesha mvua na huku Mtume anatoa Khutbah siku ya Ijumaa na hakujumuisha pamoja na ´Aswr. Alitoka na mvua inanyesha, lakini pamoja na hivyo hakujumuisha pamoja na ´Aswr. Hii ndio dalili ya wazi kabisa katika masuala haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-5-23.mp3
  • Imechapishwa: 09/11/2014