Dalili inayotumiwa na Suufiyyah juu ya ukitaji

Suufiyyah walioputuka mipaka wametumia dalili kwa Hadiyth hii – yaani Hadiyth ya 38 an-Nawawiyyah – juu ya masuala ya Allaah kukita katika kila kiumbe. Kuna upokezi uliyoundwa uliyozidishwa katika Hadiyth hii baada ya neno:

“… mikono yake ambayo anakamatia, miguu yake anayoendea”

Wakaongeza:

“Mpaka anakiambiwa kitu: “Kuwa!” na kinakuwa”.”

Upokezi huu unapatikana katika baadhi ya vitabu vya Hadiyth vilivyoandikwa. Lakini hata hivyo ni upokezi uliyoundwa.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 511
  • Imechapishwa: 10/05/2020