Daktari anahisi matamanio anapowatibu wanawake

Swali: Nafanya kazi kama daktari katika taasisi ya udaktari na huwafunua wanamme na wanawake. Hutokea wakati mwingine wakati ninapofanya kazi yangu na wanawake yakaamka matamanio yangu pamoja na kwamba napambana na jambo hilo. Jambo hili hunitokea mara nyingi. Ni ipi hukumu ya wudhuu´ wangu nikiwa katika hali hii? Unaninasihi nini?

Jibu: Haijuzu kwako kuwafunua wanawake. Haijuzu kwa mwanamme kuwafunua wanawake hata kama hayakuamka matamanio yako. Kwa sababu hiyo ni njia inayopelekea katika fitina. Wanawake wafunuliwe na madaktari wanawake wenzao. Wanamme wafunuliwe na madaktari wanamme wenzao. Haijuzu kinyume chake. Kwa sababu jambo hilo ndani yake mna fitina. Matamanio yakiamka basi jambo linakuwa baya zaidi. Ikiwa matamanio yameambatana na kugusa ngozi ya mwanamke pasi na kizuizi kitendo hicho kinachengua wudhuu´. Kumgusa mwanamke kwa matamanio kunachengua wudhuu´ ikiwa ni moja kwa moja pasi na kuzuizi. Kwa hali yoyote usifanye kazi hii. Jiepushe na kazi hiyo. Fanya kazi yako na wanamme tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=1Aulyc_Efzo
  • Imechapishwa: 26/03/2022