Swali: Unasemaje kazi ya daktari mara nyingine anahitajia kutazama uchi wa mgonjwa au kuugusa kwa ajili ya kipimo na wakati mwingine katikati ya operesheni daktari anafanya upasuaji kwa katikati ambapo pamejaa damu na mkojo. Je, katika hali kama hii ni lazima kurudi kutawadha upya au ni kwa minajili ya ubora tu?

Jibu: Hakuna neno kwa daktari kugusa uchi wa mwanamme kutokana na haja na akautazama kwa sababu ya matibabu. Ni mamoja uchi huo ni tupu ya mbele au ya nyuma. Inafaa kwake kutazama na kugusa kutegemea na haja na dharurah. Vilevile ni sawa akagusa damu kwenye jeraha kutokana na haja ili kulitibu au kujua hali ya jeraha. Baada ya hapo ataosha mikono yake yale maeneo yaliyopatwa.

Wudhuu´ hauchenguki kwa kugusa damu au mkojo. Lakini akigusa tupu basi wudhuu´ wake unachenguka ni mamoja ni tupu ya mbele au tupu ya nyuma.

Kuhusu kugusa damu, mkojo au najisi nyenginezo hakuchengui wudhuu´. Lakini hata hivyo ataosha yale maoneo yaliyopatwa. Lakini yule mwenye kugusa tupu pasi na kizuizi akagusa ngozi kwa ngozi basi wudhuu´ wake unachenguka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule atakayeingiza mkono wake kwenye tupu yake na hakuna chini yake sitara, basi wudhuu´ umemuwajibikia.”

Vivyo hivyo daktari akigusa tupu ya mwanamke kutokana na haja basi wudhuu´ wake unachenguka kwa kitendo hicho akiwa na twahara kama mwanamme.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/25)
  • Imechapishwa: 18/02/2021