Daktari kamshauri kutofunga lakini anag´ang´ania kufunga

Swali: Ikiwa mtu ni mgonjwa ana maradhi yasiotarajiwa kupona kama kisukari, akamnasihi daktari asifunge kwa kuwa itamuathiri afya yake siku za mbele, naye anaona yuko na uwezo wa kufunga. Ipi hukumu ya swawm yake, na je achukue wasia wa daktari ikiwa ni muislamu mwaminifu. Je, anapata dhambi ikiwa atafunga na akaja kuathirika baadaye?

Jibu: Ninavyoona – wa Allaahu ndiye mjuzi zaidi – ikiwa kweli anaona anaweza kufunga bila ya kuathirika, basi funga. Na kutokana na swawm hii itakuwa – Allaah akitaka – ndo dawa yako kwa idhini ya Allaah. Na ikiwa utafikwa na uzito [madhara], wewe Alhamdulillaah ni muislamu. Ridhika na Aliyokadiria Allaah na ule hata kama itakuwa imeshafika wakati wa mwisho ya mchana. Kula kitu chochote. Ama kujishughulisha na vyakula na raha za nafsi na hukufikwa na athari yoyote. Mshukuru Allaah Kukufikisha katika khayr na ´Ibaadah hii.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://alwasabi.al3ilm.com/alfatawaa
  • Imechapishwa: 10/05/2020