Swali: Je, Daawuud alikuwa Mtume kwa kuwa aliteremshiwa Zabuur?

Jibu: Daawuud ni mfalme na Nabii. Allaah Alimkusanyia kuwa na ufalme na utume. Sio kama anazingatiwa kuwa ni katika Mitume, ni Nabii na mfalme.

Zabuur sio kitabu cha Ahkaam. Ni kitabu cha Du´aa. Sio Ahkaam. Daawuud anahukumu kwa Tawrat iliyokuja na Muusa (´alayhis-Salaam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-03-07.mp3
  • Imechapishwa: 14/11/2014