Swali: Ipi tofauti kati ya Daar-ul-Islaam, Daar-ul-Kufr na Daar-ul-Harb?

Jibu: Daar-ul-Islaam ni nchi ambao wakazi wake wengi ni Waislamu. Hata kama kiongozi wake atakuwa ni Ishtiraakiyyah (Socialist) au hana Dini kabisa. Hii ni nchi ya Kiislamu na Daar-ul-Islaam. Ama Daar-ul-Harb ni nchi ambayo inapigana vita na Waislamu. Ama Daar-ul-Kufr ni nchi ambayo wengi wa wakazi wake ni makafiri. Daar-ul-Islaam ni tukufu na ni Haramu kupigana vita na kuua ndani yake. Ama Daar-ul-Kufr, haijuzu kuwalaghai ikiwa watu wake wameahidiwa usalama ikiwa au ikiwa kuna mkataba wa amani. Ama Daar-ul-Harb, ni kama tulivyosema. Ni ile nchi ambayo inapigana vita na Waislamu. Hali ni namna hiyo kwa mfano wakati wa sasa ambapo maadui wa Uislamu wanapiga vita Uislamu, sawa kwa njia ya moja kwa moja au kupitiaWaislamu majasusi.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.net/multimediaFiles/7615File21414.mp3
  • Imechapishwa: 22/03/2018