Chumo Halali Na Safi Kabisa


Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Riziki yangu imewekwa chini ya kivuli cha mkuki.”[1]

Nini maana yake?

Jibu: Kunamaanishwa mateka. Mateka yalikuwa ni halali kwae na hayakuwa halali kwa wengine wote kabla yake. Ni katika sifa za kipekee za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

فَكُلُوا مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Kuleni katika mlivyopata ghanima ambavyo ni halali na vizuri na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[2]

Mateka ya Jihaad ni halali na safi. Wanasema kuwa mateka ya Jihaad ndio chumo safi kabisa, kwa kuwa Allaah amesema:

حَلَالًا طَيِّبًا

“… ni halali na vizuri.”

[1] Ahmad (03/50).

[2] 08:69

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (7) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt--15041434.mp3
  • Imechapishwa: 21/03/2017