Si sahihi kumsifu Allaah kwa matendo wanayofanya viumbe. Kiumbe ndiye mwenye kufanya matendo yake kihakika kwa Allaah kumfanya akaweza kuyafanya.

Chimbuko la upotevu wa Jabriyyah utata wao wanasema kuwa mja hana matendo ili kusije kutokea katika ufalme wa Allaah asiyoyataka na kusiwe Muumba mwingine mbali na Allaah. Hili ni kinyume na wanavosema Qadariyyah.

Chimbuko la upotevu wa Qadariyyah na Jabriyyah ni kule kutotofautisha kati ya utashi (Mashiy-ah), matakwa (Iraadah), kupenda (Mahabbah), kuridhia (Ridhwaa). Chimbuko la upotevu wao ni kuwa mapote yote mawili yamefanya matashi na matakwa, kupenda na kuridhia ni kitu kimoja. Jabriyyah na Qadariyyah wemefanya hayo ni kitu kimoja kisha wakatofautiana. Matakwa kwa mujibu wa Qadariyyah ni kitu moja tu nayo ni ya kilimwengu. Ndipo wakasema ulimwengu wote umekuwa kutokana na mipango na makadirio ya Allaah na hivyo yanakuwa ni yenye kupendwa na kuridhiwa ikiwa ni pamoja na maasi na kufuru [yanapendwa na kuridhiwa pia]. Vilevile matakwa kwa mujibu wa Qadariyyah ni kitu kimoja tu nayo ni yale ya Kishari´ah. Ndipo wakasema yale aliyoyaweka Allaah katika Shari´ah basi ni mwenye kuyakadiria, kuyaamrisha, na kuyapenda. Maasi sio kitu kinachopendwa na Allaah wala kukiridhia. Hivyo hayakukadiriwa wala kupangwa. Mambo haya yanatoka katika matakwa ya Allaah na aliyoumba.

Wanapigwa Radd kwa kuambiwa kuwa tofauti kati ya utashi na kupenda ni kitu kimetolewa dalili na Qur-aan, Sunnah na maumbile sahihi.

Kuhusiana na utashi katika Qur-aan ni maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَلَوْ شِئْنَا لَآتَيْنَا كُلَّ نَفْسٍ هُدَاهَا

“Na Tungelitaka tungeliipa kila nafsi mwongozo wake.” (32:13)

تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ

“Hizo ni alama za Allaah Tunakusomea kwa haki; na hakika wewe ni miongoni mwa Mitume.” (02:252)

وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ عُدْوَانًا وَظُلْمًا فَسَوْفَ نُصْلِيهِ نَارًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا

“Na atakayefanya hivyo kwa uadui na dhulma, basi Tutamuingiza Motoni – na hilo kwa Allaah ni mepesi.” (04:30)

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ

“Na hamtoweza kutaka chochote isipokuwa Atake Allaah.” (76:30)

مَن يَشَإِ اللَّـهُ يُضْلِلْـهُ

“Yeyote Allaah amtakaye humpotoa.” (06:39)

وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا

“Na yule ambaye anataka kumpotoa, basi hufanya kifua chake kuwa na dhiki.” (06:125)

Kuhusiana na maandiko ya kupenda na kuridhia ni Kauli ya Allaah (Ta´ala):

وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ

“Na Allaah hapendi ufisadi.” (02:205)

وَلَا يَرْضَىٰ لِعِبَادِهِ الْكُفْرَ

“Na wala haridhii kufuru kwa waja Wake.” (39:07)

كُلُّ ذَٰلِكَ كَانَ سَيِّئُهُ عِندَ رَبِّكَ مَكْرُوهًا

“Yote hayo uovu wake daima ni wa kukirihisha mbele ya Mola wako.” (17:38)

Yanakabiliwa na yale aliyokataza; shirki, dhuluma, machafu na kiburi. Vilevile imekuja katika Hadiyth:

“Allaah amechukia kwenu mambo matatu; porojo, kuuliza sana na kuharibu mali.” al-Bukhaariy (1477), Muslim (593).

Katikatika “al-Musnad” imekuja:

“Allaah anapenda zichukuliwe rukhusa zake kama kama anavochukia kuendewa maasi yake [aliyokataza].” Ahmad (04/108) na Ibn Hibbaan (2742).

Madhehebu ya Ahl-us-Sunnah ni kwamba utashi na kupenda sio kitu kimoja na sio mambo mawili yenye kulazimiana. Allaah anaweza kutaka kitu asichokipenda na akapenda kitu ambacho hataki kitokee.

Mfano wa kwanza ni kama kutaka Kwake kupatikana Iblisi na jeshi lake na matakwa yake yaliyoeenea juu ya kila kilichoko ulimwenguni na wakati huo huo akawa anachukia baadhi ya vitu hivyo. Mfano wa pili ni kama kupenda kwake imani kwa makafiri na watenda maovu na lau angelitaka hilo angelifanya yote hayo. Kwani aliyoyataka yamekuwa na asiyoyataka hayakukua. Mapote haya mawili yanaraddiwa kwa Kauli ya Allaah (Ta´ala):

وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ

“Allaah amekuumbeni na yale mnayoyatenda.” (37:96)

Bi maana amekuumbeni na yale mnayoyafanya. Hii ni dalili yenye kuonesha kuwa matendo ya waja yameumbwa na Allaah na wakati huo huo ni matendo yao ya kihakika. Hapa kuna Radd kwa Jabriyyah wanaosema kuwa mja ametenzwa nguvu. Kadhalika kuna Radd kwa Qadariyyah wenye kusema kuwa mja ni mwenye kujiumbia matendo yake mwenyewe kivyake. Vilevile wanaraddiwa kwa Hadiyth ya Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh):

“Allaah ameumba kila mtendaji na matendo yake.” Ameipokea al-Bukhaariy katika “Khalq Af´aal-il-´Ibaad” (01/46).

Allaah amemuumba mwanaadamu pamoja na mambo yake yote kukiwemo harakati anazofanya.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/360-363)
  • Imechapishwa: 21/05/2020