Chimbuko la jina Raafidhwah


Swali: Waliopetuka katika kumpenda ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) wanaitwa Shiy´ah au Raafidhwah?

Jibu: Kupetuka mipaka hakujuzu, sawa kwa kumpenda ´Aliy wala mwingine. Upetukaji mipaka haujuzu. Linalotakikana ni ukati na kati baina ya uchupaji mipaka na uchujaji. Wenye kusema kuwa ´Aliy ndiye anastahiki uongozi na kwamba yeye ndiye aliyeacha anausia baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hawa ndio Shiy´ah. Wenye kuitwa Raafidhwah ni Ja´fariyyah. Wanaitwa Raafidhwah kwa kuwa walimkataa Zayd bin ´Aliy wakati walipomuuliza kuhusu Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na akawa amewasifu na kuwatapa. Hivyo wakawa wamesema:

“Tunakukataa.”

Hapo ndipo waliitwa Raafidhwah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_12.mp3
  • Imechapishwa: 22/06/2018