Swali: Mwezi wa Ramadhaan unakuja na wanafunzi wa kiume na wa kike wameshughulishwa na kufanya mazoezi kwa ajili ya mitihani na sehemu kubwa ya mwezi huu itamalizikia katika mitihani hii na mazoezi mbali na wanafunzi wa chuo kikuu. Ni zipi nasaha zako kwa vile tutashughulishwa kutokamana na kisomo cha Qur-aan na huenda vilevile tukapitwa na Tarawiyh na Nawaafil? Ni vipi mtu atayakusanya hayo?

Jibu: Kwanza kuhusu wanawake nimeelezwa na raisi mkuu kwamba mitihani yao itaanza siku ya tatu ya Ramadhaan na kwamba kuhusu durusi kila siku kutakuwa darsa moja tu. Jambo hili halimshughulishi mwanamke kiasi cha kwamba asiweze kusimamisha Ramadhaan. Ajifanyie wepesi nafsi yake.

Ama kuhusu wanaume yule ambaye ni mwenye kujitahidi mwanzoni mwa mwezi basi hatohitajia kufanya mazoezi mengi. Yule mwenye kufanya upuuzi basi ameifanyia upuuzi nafsi yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1596
  • Imechapishwa: 17/03/2020