Chakula cha jioni kwa mfanyakazi wa benki

Swali: Nina rafiki ambaye ni kafiri amenialika kula chakula cha jioni. Lakini hata hivyo anafanya kazi katika benki ya ribaa. Je, inafaa kwangu kuitikia mwaliko wake ikiwa anafanya kazi katika benki hii ya ribaa?

Jibu: Ikiwa unajua kuwa chakula alichopika kinatokana na pesa ya haramu, basi usikile. Lakini ikiwa kipato chake kimechanganyikana na pesa ya halali na pesa ya haramu, kula. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikula katika chakula cha mayahudi ilihali wanatumia ribaa. Kwa sababu hakuwa na uhakika kuwa chakula hicho kimepikwa na pesa ya ribaa au na pesa ya haramu. Lakini mtu ambaye hana kipato kingine isipokuwa tu cha haramu, usile katika chakula chake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (29)
  • Imechapishwa: 11/02/2022