Cha kufanya kwa ambaye aliwakosea wazazi wake zamani

Swali: Ni vipi nitawafurahisha wazazi wangu ambao hivi sasa wanaishi kwa sababu hapo kabla nilikuwa nawakasirisha na kuwadhikisha namna nilivyokuwa natangamana nao?

Jibu: Muda wa kuwa umetubia kwa Allaah, tangamana nao vyema na uwahudumie, zungumza nao kwa uzuri, kaa nao, watatulie mahitaji yao na wasaidie yale mambo yao muhimu ya dunia. Pengine kwa kufanya hivo Allaah akakusamehe yale yaliyotangulia.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/فتاوى-على-الهواء-19-12-1435هـ
  • Imechapishwa: 19/06/2022