Bwanyenye amejenga msikiti na kuusia azikwe ndani yake

Swali: Kuna mwanaume amejenga msikiti na akaacha anausia azikwe ndani yake ambapo ukatekelezwa wasia wake. Hivi sasa watu wafanye nini?

Jibu: Wasia huu wa kuzikwa msikitini sio sahihi. Misikiti sio makaburini na wala haijuzu kuzika msikitini. Ni haramu kutekeleza wasia huu. Lililo la wajibu hivi sasa ni kufukua kaburi hili na kulipeleka katika makaburi ya waislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/233)
  • Imechapishwa: 04/06/2017