Swali: Mtoto wangu wa kiume ameoa pasi na ushauri wangu. Matokeo yake nikamfukuza nyumbani kwangu. Je, napata dhambi kwa kuzingatia kwamba siwezi kuwahudumia?

Jibu: Umefanya makosa kumfukuza nyumbani, kwa sababu hakufanya jambo lenye dhambi. Ameoa, jambo ambalo Allaah amemhalalishia na akamwekea katika Shari´ah jambo hilo. Hakufanya jambo lenye dhambi mpaka umfukuze nyumbani. Baya linaloweza kusemwa ni kuwa hakukushauri. Lakini msamehe na puuzilia mbali. Lakini hili lisipelekee kumfukuza nyumbani.

Kuhusu matumizi ikiwa huwezi kumhudumia, basi Allaah haikalifishi nafsi zaidi ya vile inavoweza. Afanye kazi na kujaribu kujihudumia yeye mwenyewe na mke wake. Akiwa anaweza kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=PeeP5yfHfqM
  • Imechapishwa: 05/03/2022