Swali: Baadhi ya watu siku ya ijumaa wanaomba bwana wa du´aa ya msamaha[1]. Je, ni kitu kina msingi mahali hapa?

Jibu: Hakukupokelewa kitu. Lakini aombe anachotaka kati yake yeye na nafsi yake. Ni mamoja du´aa hiyo au nyingine. Lakini mahali hapa hakukupokelewa kitu maalum cha kuomba kati ya Khutbah mbili. Hata hivyo mtu akiiomba kimyakimya kati ya Khutbah mbili hapana vibaya.

[1] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Bwana wa Du´aa ya msamaha ni:

اللهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لا إِلهَ إِلاَّ أَنْتَ خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ وَأَنا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ أَبوءُ لَكَ بِنِعْمَتِك عَلَيَّ وأَبوءُ بِذَنْبِي فاغْفِرْ لي فإِنَّه لاَ يغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ

“Ee Allaah! Wewe ni Mola wangu. Hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Wewe. Umeniumba mimi na mimi ni mja wako. Nami niko juu ya ahadi Yako na agano lako kiasi cha uwezo wangu. Najikinga Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya. Nakiri Kwako kwa kunineemesha. Nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unisamehe kwani hasamehi madhambi isipokuwa Wewe.”

Mwenye kuisoma pindi inapoingia jioni na akafa usiku huo huo anaingia Peponi. Mwenye kuisoma pindi inapoingia asubuhi na akafa mchana huo huo anaingia Peponi. (al-Bukhaariy (6306).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21592/ما-المشروع-قوله-بين-خطبتي-الجمعة
  • Imechapishwa: 27/08/2022