Bora waswali mkusanyiko wao upya au wajiunge pamoja na imamu?


Swali: Watu wawili waliingia na wakamkuta imamu katika Tashahhud ya mwisho. Bora wajiunge nao katika swalah au wasubiri mpaka kutolewe salamu na waswali swalah upya?

Jibu: Wakiwa wawili au watatu na wamekuja na kumkuta imamu katika Tashahhud basi wako na khiyari; wakitaka wanaweza kujiunga pamoja na imamu na wakitaka wanaweza kusubiri mpaka kutolewe salamu. Kwa sababu swalah imeisha na swalah haiwahiwi isipokuwa kwa Rak´ah moja. Kwa hiyo wako na khiyari. Ama akiwa ni mtu mmoja asisubiri. Ajiunge pamona na imamu. Asisemi kuwa eti anasubiri mpaka aje mwengine na huenda huyo mwingine asije. Wakiwa wawili au zaidi basi wako na khiyari. Akiwa ni mmoja ajiunge pamoja na imamu japokuwa ni katika Tashahhud ya mwisho. Asisubiri. Hapana shaka kwamba wanapata thawabu za kuswali kwa mkusanyiko. Lakini ule mkusanyiko wa kwanza una ubora wake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 22/05/2019