Bora ni kuwatahadharisha Ahl-ul-Bid´ah kwa majina yao

Swali: Je, katika mfumo wa Salaf ni kutaja majina ya wale Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal ambao wanatahadharisha nao? Je, hili linakuwa kwa njia ya kudumu au inaweza kinyume na hivyo kutegemea na hali?

Jibu: Hili linategemea na manufaa. Ikiwa manufaa yanapelekea kutomlenga mtu yule basi asimlenge moja kwa moja. Ikiwa manufaa yanapelekea kumlenga kwa njia ya kwamba analingania na anaeneza Bid´ah zake katika batili, basi amtahadharishe kwa dhati yake. Akiweza kumlenga kabisa ndio bora zaidi. Leo wanaeneza magazeti na kanda ili kuwapoteza watu. Zitahadharishwe Bid´ah zao. Leo kuna walinganizi kwenye TV, magazeti na kwenginepo ambapo wana uchanganfu kwelikweli. Bora zaidi ni yeye kuwatahadharisha kwa kuwalenga. Kwani manufaa yanapelekea kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda: as-Sayr ´alaa Manhaj-is-Salaf http://rabee.net/ar/questions.php?cat=26&id=617
  • Imechapishwa: 10/03/2018