Bora ni kuwapa Zakaat-ul-Fitwr mafukara wa mji wako


Swali: Niliituma Zakaat-ul-Fitwr yangu kwenda kwa familia yangu Misri ili waitoe katika nchi yangu ilihali mimi naishi Saudi Arabia. Je, kitendo hichi ni sahihi?

Jibu: Hakuna neno kwa kufanya hivo na inasihi – Allaah akitaka – kutokana na maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Lakini kuitoa katika sehemu ambayo unaishi ndio bora na salama zaidi. Ukiituma kwa familia yako ili wawape mafukara wa mji wako pia ni sawa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/215)
  • Imechapishwa: 12/06/2018