Bora ni kuswali kwa kufupisha safarini


Swali: Tunatumai utatuwekea wazi hukumu za swalah safarini katika kufupisha na kukusanya khaswa ukizingatia kwamba watu wengi huenda likawatatiza jambo hili.

Jibu: Kuhusu kufupisha safarini ni Sunnah iliokokotezwa ambayo haitakikani kwa mtu kuiacha. Isipokuwa yule ambaye ametua katika mji anapaswa kuswali pamoja na mkusanyiko.

Ama kukusanya bora kwa msafiri akusanye pale anapokuwa barabarani bado anasafiri. Lakini akiwa ameshatua bora ni yeye kutokusanya. Ikiwa atakusanya hakuna neno kwake. Lakini mtu akiswalishwa na mtu anayeswali kikamilifu, basi ni lazima kwake kuswali kikamilifu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yale mtakayowahi swalini na yale yaliyokupiteni yakamilisheni.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (73) http://binothaimeen.net/content/1709
  • Imechapishwa: 17/04/2020