Bora ni kuleta Adhkaar kwa vidole


Swali: Ni ipi hukumu ya kusabihi kwa Tasbiyh na kuomba Istighfaar nayo pamoja na kujua kuwa inasaidia sana?

Jibu: Haina haja. Vidole ni bora zaidi. Sabihi kwa vidole. Hili ndio bora zaidi. Vilevile unaweza kusabihi kwa vijiti, hivi ndivyo alivyofanya Juwayriyah bint Haarith ambaye ni mama wa waumini (Radhiya Allaahu ´anhaa). Hesabu kwa vijiti au vidole.

Ama kuhusiana na Tabsiyh leo imekuwa ni alama ya Suufiyyah. Wanaitakidi kuwa ina fadhila na kwamba imewekwa katika Shari´ah. Usijifananishe nao. Jengine ni kwamba huna haja nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14005
  • Imechapishwa: 18/04/2018