Bora ni kufunga jumatatu na alkhamisi au siku tatu kila mwezi?

Swali: Ni lipi bora; kufunga jumatatu na alkhamisi au siku tatu kila mwezi?

Jibu: Akifunga jumatatu na alkhamisi amefunga siku tatu za mwezi bali na zaidi. Atakuwa amefunga siku ngapi kwa mwezi akifunga jumatatu na alkhamisi? Siku nane. Kufunga jumatatu na alkhamisi kunamtosheleza mtu kufunga siku tatu. Lakini kufunga siku tatu kwa mwezi hakumtoshelezi mtu na funga ya jumatatu na alkhamisi. Kwa hivyo afunge swawm ya jumatatu na alkhamisi. Lakini akiweza kuongeza juu yake funga ya masiku meupe ndio bora.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (56) http://binothaimeen.net/content/1288
  • Imechapishwa: 11/10/2019