Bora mchana wa Ramadhaan kusoma Qur-aan au swalah ya sunnah?

Swali: Ni kipi kati ya mambo mawili bora zaidi mchana wa Ramadhaan; kusoma Qur-aan au swalah ya sunnah?

Jibu: Ilikuwa ni katika mwongozo wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mchana wa Ramadhaan kufanya ´ibaadah kwa wingi na Jibriyl alikuwa akimfunza Qur-aan usiku. Jibriyl alipokuwa akutana naye basi alikuwa ni mkarimu zaidi juu ya mambo ya kheri kuliko upepo uliotumwa. Alikuwa ndiye mkarimu zaidi wa watu na alikuwa anakuwa mkarimu zaidi katika Ramadhaan. Alikuwa anakithirisha zaidi swadaqah, kutenda wema, kusoma Qur-aan, kuswali, Dhikr na kufanya I´tikaaf. Huu ndio mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mwezi huu na katika mwezi huu mtukufu.

Kuhusu ubora kati ya kisomo cha msomaji na swalah ya sunnah ya mswaliji, ni kitu kinatofautiana kutegemea na zile hali za watu. Makisio ya hayo yanarejea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa sababu Yeye amekizunguka kila kitu kiujuzi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/363)
  • Imechapishwa: 07/11/2021