Bora kwa mwanamke atulizane nyumbani


Swali: Ni ipi hukumu ya kisomo cha Qur-aan cha pamoja cha wanawake msikitini kwa ajili ya kujifunza na kuirejea? Ikiwa haijuzu, wasichana waache kwenda msikitini kwa jambo hilo?

Jibu: Hapana shaka kwamba kimsingi mwanamke anakuwa nyumbani sawa wakati anaposwali au kwa ajili ya kujifunza Qur-aan. Ama tukiwazoweza kutoka nje kwa ajili ya kujifunza Qur-aan au kitu kingine, mwishowe itawapelekea kupuuza kubaki majumbani. Mimi naona kuwa msingi ni kwamba wanawake wasome na waswali majumbani. Pia ndio kunawahifadhi vyema zaidi. Hivi sasa wamekuwa wanawatoa wanawake nje. Mwanamke anapenda kutoka nje, kwenda na kurudi. Hivi sasa nyinyi wenyewe ndio mnawafungulia milango. Wamekuwa hawazijui tena nyumba zao na wanajenga hoja kwamba wanasoma na hili na lile. Mimi naona bora kuwa ni kuacha kufanya hivo na badala yake wabaki majumbani. Kile wanachojifunza huko kinatosha – Allaah akitaka. Hakuna haja wabobee katika masuala fulani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=BUF_eRJJ0VE&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 13/04/2020