Bora kwa mwanamke aswali Tarawiyh nyumbani

Swali: Ni bora kwa mwanamke kuswali Tarawiyh nyumbani au msikitini?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwazuie wajakazi wa Allaah na Misikiti ya Allaah. Majumba yao ni bora kwao.”

Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba ni bora kwake kuswali nyumbani. Lakini akienda msikitini kwa nia nzuri ni kitendo kizuri. Hata hivyo atoke hali ya kuwa ni mwenye kujiheshimu; asiwe ni mwenye kujipamba na kujitia manukato. Hakutoka ili ajionyeshe. Ametoka kufanya ´ibaadah. Atoke kwa heshima na kwa Hijaab. Aingie Msikitini na dada zake na aswali na Waislamu wengine. Ni kitendo kizuri sana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo%20%20-%2021%20-%2008%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015