Bora kwa mwanamke aswali misikiti Mitakatifu au nyumbani kwake?


Swali 289: Kuhusu wanawake wanaofanya ´Umrah katika Ramadhaan – je, bora kwao kuswali kwenye majumba yao au kuswali kwenye msikiti Mtakatifu? Ni mamoja iwe inahusiana na faradhi au Tarawiyh?

Jibu: Sunnah imefahamisha kwamba bora kwa mwanamke ni yeye kuswali nyumbani kwake. Haijalishi kitu ni pahali gani. Ni mamoja iwe Makkah au kwengine. Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwazuie wajakazi wa Allaah kutokamana na misikiti ya Allaah – na nyumba zao ni bora kwao.”

Aliyasema hayo pamoja na kwamba yuko Madiynah. Pamoja na kwamba msikiti wa Mtume una fadhilah za zaidi. Jengine ni kwa kuwa swalah ya mwanamke kwenye nyumba yake ni sitara zaidi kwake na ni jambo linalomweka mbali zaidi na fitina. Hivyo ikawa swalah yake nyumbani kwake ndio bora na kuzuri zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthyamiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 110
  • Imechapishwa: 10/10/2019